Забур 69 – CARS & NEN

Священное Писание

Забур 69:1-6

Песнь 69

(Заб. 39:14-18)

1Дирижёру хора. Песнь Давуда. В напоминание.

2Всевышний, скорее избавь меня!

Поспеши мне на помощь, Вечный!

3Пусть все, кто желает моей смерти,

будут пристыжены и посрамлены.

Пусть все, кто хочет моей погибели,

в бесчестии повернут назад.

4Пусть возвратятся со стыдом

говорящие мне: «Ага! Ага!»

5Пусть ликуют и радуются о Тебе

все ищущие Тебя,

Пусть те, кто любит Тебя за Твоё спасение,

всегда говорят: «Велик Всевышний!»

6Я же беден и нищ.

Поспеши ко мне, Всевышний!

Ты – помощь моя и мой избавитель;

Вечный, не замедли!

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Zaburi 69:1-36

Zaburi 69

Kilio Cha Kuomba Msaada Wakati Wa Dhiki

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Yungiyungi.” Zaburi ya Daudi.

169:1 Za 42:7; 32:6; Yon 2:5Ee Mungu, niokoe,

kwa maana maji yamenifika shingoni.

269:2 Ay 30:19Ninazama kwenye vilindi vya matope,

pasipo mahali pa kukanyaga,

Nimefika kwenye maji makuu,

mafuriko yamenigharikisha.

369:3 Za 6:6; 119:82Nimechoka kwa kuomba msaada,

koo langu limekauka.

Macho yangu yanafifia,

nikimtafuta Mungu wangu.

469:4 Yn 15:25; Za 25:19; 35:19; 38:19; 40:14; 119:95; Isa 32:7Wale wanaonichukia bila sababu

ni wengi kuliko nywele za kichwa changu;

wengi ni adui kwangu bila sababu,

wale wanaotafuta kuniangamiza.

Ninalazimishwa kurudisha

kitu ambacho sikuiba.

569:5 Za 38:5; 44:21Ee Mungu, wewe unajua upumbavu wangu,

wala hatia yangu haikufichika kwako.

6Ee Bwana, ewe Bwana Mwenye Nguvu Zote,

wakutumainio wasiaibishwe

kwa ajili yangu;

wakutafutao wasifedheheshwe kwa ajili yangu,

Ee Mungu wa Israeli.

769:7 Yer 15:15; Za 39:8; 44:15Kwa maana nimestahimili dharau kwa ajili yako,

aibu imefunika uso wangu.

869:8 Ay 19:13-15; Za 31:11; 38:11; Isa 53:3; Yn 7:5Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu,

mgeni kwa wana wa mama yangu mwenyewe.

969:9 Yn 2:17; Rum 15:3; Za 89:50-51Kwa kuwa wivu wa nyumba yako unanila,

matukano ya wale wanaokutukana yameniangukia.

1069:10 Za 35:13Ninapolia na kufunga,

lazima nivumilie matusi.

1169:11 2Sam 3:31; Za 35:13Ninapovaa nguo ya gunia,

watu hunidharau.

1269:12 Mwa 18:1; 23:10; Ay 30:9Wale wanaoketi mlangoni wananisimanga,

nimekuwa wimbo wa walevi.

1369:13 Isa 49:8; 2Kor 6:2; Za 17:7; 51:1Lakini Ee Bwana, ninakuomba,

kwa wakati ukupendezao;

katika upendo wako mkuu, Ee Mungu,

unijibu kwa wokovu wako wa hakika.

1469:14 Za 69:2; 144:7Uniokoe katika matope,

usiniache nizame;

niokoe na hao wanichukiao,

kutoka kwenye vilindi vya maji.

1569:15 Za 36:6; 68:22; Hes 21:33; Yer 22:2069:15 Za 28:1; 124:4, 5; Hes 16:33Usiache mafuriko yanigharikishe

au vilindi vinimeze,

au shimo lifumbe kinywa chake juu yangu.

1669:16 Za 63:3Ee Bwana, unijibu, kwa wema wa upendo wako;

kwa huruma zako nyingi unigeukie.

1769:17 Za 22:24; 143:7; 50:15; 66:14Usimfiche mtumishi wako uso wako,

uharakishe kunijibu, kwa sababu niko katika shida.

1869:18 Za 49:15Njoo karibu uniokoe,

nikomboe kwa sababu ya adui zangu.

1969:19 Za 22:6Unajua jinsi ninavyodharauliwa,

kufedheheshwa na kuaibishwa,

adui zangu wote unawajua.

2069:20 Ay 16:2; Isa 63:5; Za 142:4Dharau zimenivunja moyo

na nimekata tamaa,

nimetafuta wa kunihurumia, lakini sikumpata,

wa kunituliza, lakini sikumpata.

2169:21 Hes 6:3; Lk 23:36; Mt 27:34, 48; Mk 15:23, 36; Yn 19:28-30Waliweka nyongo katika chakula changu

na walinipa siki nilipokuwa na kiu.

2269:22 1Sam 28:9; Ay 18:10Meza iliyoandaliwa mbele yao na iwe mtego,

nayo iwe upatilizo na tanzi.

2369:23 Rum 11:9-10Macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona,

nayo migongo yao iinamishwe daima.

2469:24 Za 79:6; Yer 10:25Uwamwagie ghadhabu yako,

hasira yako kali na iwapate.

2569:25 Law 26:43; Mt 23:38; Mdo 1:20Mahali pao na pawe ukiwa,

wala asiwepo yeyote atakayeishi katika mahema yao.

2669:26 Ay 19:22; Zek 1:15Kwa kuwa wanawatesa wale uliowajeruhi,

na kuzungumza juu ya maumivu ya wale uliowaumiza.

2769:27 Neh 4:5; Za 109:14Walipize uovu juu ya uovu,

usiwaache washiriki katika wokovu wako.

2869:28 Kut 32:32-33; Lk 10:20; Eze 13:9Wafutwe kutoka kitabu cha uzima

na wasiorodheshwe pamoja na wenye haki.

2969:29 Za 20:1Mimi niko katika maumivu na dhiki;

Ee Mungu, wokovu wako na unihifadhi.

3069:30 Za 28:7; 34:3Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo,

nami nitamtukuza kwa kumtolea shukrani.

3169:31 Za 50:9-13; 51:16Hili litampendeza Bwana kuliko ngʼombe dume,

zaidi ya fahali akiwa na pembe na kwato zake.

3269:32 Za 34:2; 22:26Maskini wataona na kufurahi:

ninyi mnaomtafuta Mungu, mioyo yenu na iishi!

3369:33 Za 12:5Bwana huwasikia wahitaji

wala hadharau watu wake waliotekwa.

3469:34 Za 96:11; 98:7; Isa 44:23Mbingu na dunia zimsifu,

bahari na vyote viendavyo ndani yake,

3569:35 Oba 1:17; Ezr 9:9; Za 51:18kwa maana Mungu ataiokoa Sayuni

na kuijenga tena miji ya Yuda.

Kisha watu watafanya makao yao humo na kuimiliki,

3669:36 Za 25:13; 37:29watoto wa watumishi wake watairithi

na wale wote walipendao jina lake

wataishi humo.